Raia wa Marekani akamatwa Korea Kaskazini

Msukosuko ni mkubwa kufuatia maonyesho makubwa ya zana za kivita Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msukosuko ni mkubwa kufuatia maonyesho makubwa ya zana za kivita

Shirika la habari la Korea Kusini linasema kwamba raia wa tatu wa Marekani ametiwa mbaroni nchini Korea Kaskazini.

Bila kutaja vyanzo vyake, shirika hilo linasema mwanamume huyo mwenye asili ya kimarekani na kikorea alikamatwa akiwa kwenye uwanja wa ndege akijaribu kuondoka Pyongyang.

Inaarifiwa kwamba mwanamume huyo ni mhadhiri wa zamani wa chuo kikuu cha Yanbian Uchina, na alikuwa korrea kaskazini kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa shughuli za uhisani.

Serikali za korea kusini na kaskazini hazijadhibitisha madai hayo.

Raia wengine wawili wa Marekani wanazuiliwa nchini humo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Korea Kaskazini ilifanya maonyesho makubwa ya za za kivita