Mwandishi maarufu Kuki Gallmann apigwa risasi na kujeruhiwa Kenya

Kuki Gallmann Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hoteli ya kifahari inayomilikiwa na Bi Gallmann ilichomwa moto mwezi uliopita

Watu waliojihami na bunduki wamempiga risasi na kumjeruhi mwanamazingira na mwandishi mzoefu mzaliwa wa Italia, Kuki Gallmann.

Amepigwa risasi ya tumbo akiwa kwenye shamba lake kaunti ya Laikipia.

Mwezi uliopita makahawa wake wa kifahari uliteketezwa na watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji.

Bi Gallmann, amekuwa mwenyeji wa Kenya tangu miaka ya sabini, na anafahamika zaidi kutokana na kitabu chake 'I Dreamed of Africa'.

Filamu ya kitabu hicho pia ilitolewa, mhusika mkuu, akiwa mwigizaji maarufu wa Marekani , Kim Basinger.

Haki miliki ya picha The Star, Kenya
Image caption Mwezi uliopita makahawa wa Bi Gallmann uliteketezwa na wafugaji
Image caption Laikipia