Wakenya watawala mbio za London Marathon

Mary Keitany Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mary Keitany

Wakenya Mary Keitany na Daniel Wanjiru wameibuka washindi wa mbio za London Marathon.

Keitany ameandikisha rekodi mpya ya wanawake pekee katika mbio za nyika kwa muda wa 2:17:01.

Amechukua taji hilo kwa mara ya tatu sasa akiwa na miaka 35.

Mke na mumewe kutoka Kenya washinda mbio za Paris Marathon

Mkenya Peres Jepchirchir aweka rekodi marathon

Wakenya watawala mbio za Boston Marathon

Muithiopia Tirunesh Diababa amemaliza katika nafasi ya pili kwa muda wa 2:17:56

Katika mbio za wanaume Daniel Wajiru wa Kenya ameshinda kwa muda wa 2:05:56 na kufuatwa kwa karibu na Kenenisa Bekele wa Ethiopia

Image caption Kenenisa Bekele (kushoto) na Daniel Wanjiru