Msichana wa miaka 8 aeleza alivyonusurika ajali ya kuzama kwa gari

Chloe (chini kushoto) alinusurika lakini mamake, ndugu na dadake walifariki Haki miliki ya picha facebook
Image caption Chloe (chini kushoto) alinusurika lakini mamake, ndugu na dadake walifariki

Msichana wa umri wa miaka 8 ambaye alinusurika wakati gari alimokuwa lilizama na kuwaua watu watatu wa familia ameelezea alivyojikakamua kujiokoa.

Chloe Kabealo anasema alifungua mshibi na akajaribu kupanda kupata hewa ndipo akapata fursa ya kuelea.

Chloe mama yake ,dada yaka na nduguye walikuwa ndani ya gari katika mjio wa Tumbulguni wakati liliteleza na kutumbukia kwenye mto uliokuwa na maji mengi mapema mwezi huu.

Chloe alifanikiwa kujiokoa na kukimbia kwa nyumba moja kutoa habari

Mama yao Stephanie King mwenye umri wa maiak 43, alikufa wakati akijaribu kuwaokoa watoto wake.

Mwanamke huyo alipatikna akiwa amefariki huku akimshika mtoto wake ishara kuwa alijaribu kuwaokoa watoto kabla hajafariki.

Ella Jane, mwenye umri wa miaka 11, na Jacob mwenye uri wa miaka 7 walifariki.