Arsenal yaifuata Chelsea fainali ya FA kwa kulaza Manchester City

Arsenal Haki miliki ya picha PA
Image caption Wachezaji wa Arsenal wakishangalia goli la ushindi

Washika mitutu wa London klabu ya Arsenal imetinga fainali ya kombe la kombe Fa baada ya kuwachapa Manchester City kwa mabao 2-1 .

Mchezo huo wa nusu fainali ulichukua dakika 120 baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa sare ya bao 1-1 katika dakika tisini za muda wa kawaida.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Sergio Aguero akishangilia goli la kuongoza la alilolifunga

Man City ndio walioanza kuzifumani nyavu za Arsenal kwa goli la dakika ya 62 liliowekwa kambani na mshambuliaji wake mahiri Sergio Aguero Kun.

Beki wa kushoto wa Arsenal Nacho Monreal alisawazisha bao lilo katika dakika ya 71 ya mchezo .

Alexis Sanchez aliipeleka timu yake fainali kwa goli alilofunga katika dakika ya 101, kwa kufuatia patashika ya mpira wa kutengwa iliyotokea kwenye goli la City.

Fainali ya mchezo wa kombe la FA utapigwa Mei 27 katika dimba la Wembley ambapo Arsena watakipiga na Chelsea kuwania ubingwa wa kikombe hicho.