Barcelona waichapa Madrid El Clasico

Barca Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Lionel Messi baada ya kuifunga Real Madrid

Miamba ya soka ya Hispania klabu ya Barcelona, wameibuka kidedea katika mchezo wa El Clasico, kwa kuichapa Real Madrid kwa mabao 3-2.

Kiungo wa Kibrazil Carlos Henrique Casemiro, alifunga goli la kuongoza la Real Madrid kisha Lionel Messi, akakomboa bao hilo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption James Rodrigues akishagilia goli lake la kusawazisha

Ivan Rakitic akaiongezea Barca, goli la pili katika dakika ya 73 ya mchezo kabla ya mshambuliaji James Rodriguez wa Real Madrid, kuchomoa goli katika dakika ya 86.

Katika dakika ya 90 Lionel Messi, aliifungia timu yake bao la ushindi na hivyo timu yake inarejea kilele mwa ligi wakiwa na alama 75 huku madrid wakiwa katika nafasi ya pili kwa alama 75, wakitofautiana idadi ya magoli na Real wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Madrid walicheza pungufu katika mchezo huu baada ya beki wake kisiki Sergio Ramos, kupewa kadi nyekundu.