Safaricom yakumbwa na matatizo ya mawasiliano Kenya

M-Pesa, Nairobi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hitilafu imeathiri pia M-Pesa inayotumiwa na zaidi ya watu 20 milioni

Kampuni kubwa ya mawasiliano nchini Kenya Safaricom imekumbwa na matatizo ya kiufundi ambayo yameathiri huduma zake za simu.

Safaricom imesema hitilafu hiyo imeathiri huduma zake kote nchini humo.

"Tunakabiliwa na tatizo la kuunganisha simu, data na huduma ya M-Pesa. Tatizo hili kwa sasa linaangaziwa. Samahani kwa usumbufu," kampuni hiyo imeambiwa wateja kupitia Twitter.

Jina la kampuni hiyo limeanza kuvuma katika mitandao ya kijamii, wateja wakitaka kujua nini sababu yao kushindwa kupiga simu na kupokea au kutuma pesa.

Kampuni hiyo imeesema kiini cha matatizo hayo ni hitilafu katika hifadhi data yake ya GSM, teknolojia inayofanikisha mawasiliano ya simu za rununu duniani.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya, asilimia 71.2 ya watu wanaotumia simu za rununu Kenya hutumia mtandao wa Safaricom.

Kampuni hiyo ina jumla ya wateja 27.2 milioni wa simu za rununu.

Haki miliki ya picha TWITTER
Image caption Majibu ya Safaricom kwa wateja waliokuwa wakilalamikia kampuni hiyo kwenye Twitter

Mada zinazohusiana