Nchi tatu za Afrika kupata chanjo ya kwanza ya Malaria

Zaidi ya watoto 15 wamefanyiwa majairibia ya chanjo hiyo Haki miliki ya picha D Poland/PATH
Image caption Zaidi ya watoto 15 wamefanyiwa majairibia ya chanjo hiyo

Chanjo ya kwanza kabisa duniani dhidi ya ugonjwa wa Malaria itaanza kutolewa kwa nchi tatu zikiwemo Ghana, Kenya na Malawi kuanzia mwaka 2018.

Chanjo hiyo ya RTS,S inaipa mafunzo kinga ya mwili ili iweze kusbulia viini vya Malaria ambavyo husambazwa na mbu.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa chanjo hiyo ina uwezo wa kukoa maisha ya maelfu ya watu.

Lakini bado haijabainika ikiwa inaweza kutumika kati nchi maskini zaidi duniani.

Mtu anastahili kupewa chanjo hiyo mara nne , mara moja kwa mwezi kwa muda wa miezi mitatu kabla ya kupata chanjo ya nne miezi 18 baadaye.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Zaidi ya watoto 15 wamefanyiwa majairibia ya chanjo hiyo

Mafanikio haya yamepatikana kufuatia majaribio yaliyopata ufadhili mkubwa lakini haujulikani ikwa majaribio hayo yaanaweza kufanyika katika nchi ambapo huduma za afya ni duni.

Hii ndiyo sababu WHO inaendesha majaribio hayo kati nchi tatu kubaini ikiwa mpango mzima wa utoaji chanjo hiyo unaweza kuanza

Mpango wa utoaji chanjo hiyo utawahusisha zaidi ya watoto 750,000 walio na umri wa kati ya miezi 5 na 17.