Mwanamume anayelipwa kudukua mtandao wa Twitter

Jake Davis Haki miliki ya picha Jake Davis
Image caption Jake Davis

Vijana siku wanaweza kutumbukia kweny uhalifu wa mitandao kutokana na kuwepo njia rahisi za udukuzi.

Lakini pia kuna njia ya kudukua kihalali mitandao ya kampuni na hata kulipwa kwa kufanya kazi hiyo.

Jake Davis, ambaye anajulikana mitandaoni kama Topiary, alikamatwa kwa kudukua kinyume cha sheria mwaka 2011, lakini sasa anafanya kazi hiyo hiyo kwa njia halali.

Anaeleza jinsi anavyolipwa na kampuni ya Twitter ili kudukua mtandao wao.

Haki miliki ya picha Hackerone.com
Image caption Kuna mitandao ambapo kampuni hutangaza malipo kwa wadukuzi

Udukuzi unatajwa kuwa halali wakati mdukuzi hulipwa na kampuni kudukua mtandao wao kugundua kasoro kwenye usalama wa mtandao huo.

Kisha mdukuzi hulipwa kwa kugundua kasoro ambazo baadaye hutumiwa na kampuni kuboresha usalama wa mtandao wake.

"Twiter imenilipa kwa kugundua kasoro katika mtandao wao, anasema Jake.

Kulinga na Jake, malipo makubwa kwa wadukuzi wengi ni pongezi kutoka kwa wadukuzi. Hii ni kwa sababu kuwa wao hutaka kutambuliwa kuwa walio na ujuzi kwa kazi hiyo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Udukuzi

Makampuni makubwa yanaweza kutoa malipo mazuri kwa kuwadukua, anasema Jake.

Facebok kwa mfano hulipa vizuri, wao hawalipi chini ya puini 500 kwa kuwaonyesha kasoro.

Anasema kuwa malipo ya chini zaidi ya Twitter ni dola 140 na wamewalipa wadukuzi 642 hadi sasa kwa gharama ya dola 800,000.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jake alikuwa akifanya kazi na kundi la Anonymous akidukua kinyume cha sheria