Mwanariadha mwenye miaka 101 ashinda mbio za mita 100

101-year-old Man Kaur from India celebrates after competing in the 100m sprint in the 100+ age category at the World Masters Games at Trusts Arena in Auckland on April 24, 2017. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Man Kaur celebrated her win with a little dance

Man Kaur, mwanariadha mwenye umri wa miaka 101 alishinda mbio za mita 100 wakati wa mbio za World Masters Games mjini Auckland, ambapo alisherehekea kwa kucheza densi kidogo.

Bi Kaur alimaliza mbio hizo kwa muda wa dakika moja na sekunde 14 na ndiye mwanariadha pekee kumaliza mbio hizo katika kitengo chake.

Ametajwa kama muujiza kutoka Chandigarh kwenye vyombo vya New Zealand.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Alishiriki mbio za kitengo cha watu walio na miaka 100 na zaidi

Aliruhusiwa kukimbia baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliruhusiwa kukimbia baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya

Alianza kukimbia akiwa na umri wa miaka 93 akiwa na mtoto wake wa kiume, Gurdev.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Man Kaur mwenye umri wa miaka 101 kutoka India akishereheka ushindi wake