Kijana wa mtaani mwenye ndoto ya kuunda ndege

Image caption Licha ya kutopata masomo yoyote Onyango amefanikiwa kuunda ndege hadi kufikia baadhi ya sehemu zake kuanza kufanya kazi.

Fredrick Onyango kijana wa umri wa miaka 25 huwashangaza wengi Nairobi kutokana na ndege yake ambayo licha ya kutopata masomo yoyote amefanikiwa kuiunda hadi kufikia baadhi ya sehemu zake kuanza kufanya kazi.

Onyanyo ambaye kwa miaka mingi ameishi kama mtoto wa kurandaranda mitaani mjini Nairobi maarufu kama chokoraa, alizaliwa kijiji cha Olanga huko Siaya magharibi mwa Kenya na baadaye wazazi wake wakahamia mjini Nairobi.

Huwezi kusikiliza tena
Baadhi ya sehemu za ndege zikifanya kazi

Anasema wakiwa Nairobi wazazi wake walitengana na hapo maisha yake yakachukua mkondo mwingine alipoingia mitaa ya mji angalau kujitafutia riziki.

Anasema hajafanikwa kusoma katika maisha yake yote licha ya kuoneakana kuwa na kisomo kutokana na utaalamu ambao ameonyesha katika ufundi wa kuiunda ndege yake

"Wakati nikiwa mdogo nilitazana filamu ya "Commando" ndipo nikapata motisha ya kutengeza kifaa sawa na nilichokiona katika ile filamu, nilifanikwa kuunda kifaa kile ndipo nikapata motisha ya kuunda ndege," anasema Onyango.

Image caption Licha ya kutopata masomo yoyote Onyango amefanikiwa kuunda ndege hadi kufikia baadhi ya sehemu zake kuanza kufanya kazi.

Vifaa anavyovitumia onyango kuunda ndege yake havinunui dukani bali ni vile vifaa kuu kuu ambavyo havina maana tena, vingine akivyokoa kutoka maeneo ya taka jiji.

Kisha huchukua vifaa hivyo ni kuvifanyia ukarabati na kuviunganisha pamoja hadi kufikia kiwango cha kuweza kufanya kazi kulingana na vile yeye mwenyewe anavyotaka.

Image caption Ndege hii hupata nguzu zake kutoka kwa miale ya jua

Ndege ya onyango haitumii mafuta mbali amebuni njia maalum ambapo inaweza kutumia nguvu za miale ya jua kupata nguvu za kuendesha mitambo yake.

Anasema ndege yake kwa sasa ina uwezo wa kuinuka hadi futi mbili akiongeza kuwa sheria za serikali za kumtaka awe na kibali cha kurusha ndege hiyo zimemzuia.

Image caption Licha ya kutopata masomo yoyote Onyango amefanikiwa kuunda ndege hadi kufikia baadhi ya sehemu zake kuanza kufanya kazi.

Hata hivyo Onyango anasema kuwa kinachompa changamoto kwa sasa na kukosa kusoma angalau kuweza kufahamu kwa kina zaidi programu za kompyuta, hatua ambayo ingemuezesha kupanga mifumo ya kiteknolojia ya ndege yake kwa njia inayostahili.

"Kile ambacho ningependa serikali inisaidie ni kunipeleka shule ili niweze kujifunza program ya kompuyta ambayo itaniwezesha kupanga vyema mifumo yote ya ndege yangu ili iweze kupata uwezo kamili wa kupaa," Onyango anasema.

Image caption Licha ya kutopata masomo yoyote Onyango amefanikiwa kuunda ndege hadi kufikia baadhi ya sehemu zake kuanza kufanya kazi.

Anawashauri vijana wengine walio mitaani licha ya kutosoma, watumie hekima waliyopewa na Mungu kuweza kubuni mambo ambayo yatawasaidia kuinua maisha yao.

Image caption Onyango huchukua vifaa kuu kuu ambavyo havina maana tena, vingine akivyokota kutoka maeneo ya taka jiji.