Leo ni siku ya Malaria duniani

Malaria day
Image caption Mbu

Leo ni siku ya maadhimisho ya ungojwa wa malaria duniani , nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, changa moto bado ni kubwa katika kuutokomeza ugonjwa huo kama ambavyo malengo ya shirika la afya duniani WHO lilivyo la kumaliza ungojwa huo mpaka ifikapo mwaka 2030.

Ripoti ya WHO kwa miaka miwili mfululizo 2015-2016 limebaini kwamba zaidi ya asilimia arobaini ya raia wa DRC wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa malaria.na pia kwa muujibu wa ripoti hiyo Congo na Nigeria zimekuwa nchi za kwanza duniani kuathiriwa na ugonjwa huo.

Chanjo ya kwanza ya malaria duniani itajaribiwa kwa kiwango kikubwa katika nchi ya Ghana, Kenya na Malawi kuanzia mwaka ujao.

Shirika la Afya Duniani WHO limesema chanjo hizo zinaweza kuokoa maisha ya maelfu ya maisha, huku malari ikiendelea kupoteza maisha ya watu.Mpango huo ambao uko katika majaribio utahusisha zaidi ya watoto laki saba wenye umri kati ya miezi mitano na mwaka mmoja na nusu.

Haijathibitika kwamba chanjo hiyo inaweza kufanya kazi kwa asilimia mia moja, lakini wataalamu wa masuala ya afya wanasema chanjo hiyo ni hatua muhimu katika mapambano ya dunia dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Hii inafuata miongo kadhaa ya tafiti ya kutafuta ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo duniani.

Chanjo hiyo mpya, itakwenda sambamba na hatua nyengine za kujikinga kama vile neti, dawa za kufukuza mbu, na dawa za kukinga malaria.

Wakati wa majaribio, maelfu ya watoto watapewa chanjo hiyo mara nne katika kipindi cha miaka miwili.