Hospitali yadaiwa 'kudanganya' kuhusu uzani wa mwanamke mzito

Eman Abd El Aty akiwa hisptalini baada ya kufanyiwa upasuaji Haki miliki ya picha SAIFEE Hospitali
Image caption Eman Abd El Aty akiwa hisptalini baada ya kufanyiwa upasuaji

Dadaake Eman Abd El Aty ,mwanamke wa Misri ambaye amedaiwa kuwa mzito zaidi duniani amewashutumu madaktari kwa kudanganya kuhusu uzani wake baada ya kufanyiwa upasuaji nchini India.

Alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Saifee mjini Mumbai na wiki iliopita madaktari walisema kuwa amepoteza kilo 250.

Lakini dadaake alisema kwamba ni uwongo na kwamba dadake alikuwa katika hali mbaya baada ya kukabiliwa na kiharusi.

Hospitali hiyo imekana madai hayo.

Ugomvi ulianza siku ya Jumatatu wakati dadake bi Abdi El Aty ,Shaimaa Selim alipochapisha kanda fupi ya video katika mitandao ya kijamii akidai kuwa dadake alikuwa hawezi kuzungumza ama hata kutembea na hajapoteza uzani unaodaiwa na hospitali.

Siku ya Jumanne ,aliambia BBC kwamba hospitali hiyo ilikuwa inadanganya kuhusu uzani wake.

Daktari Muffazal Lakdawala aliyeongoza opasuaji huo hakumpima uzani wake kabla na baada ya upasuaji.

Iwapo ana ushahidi wowote kuhusu kupungua kwa uzani wake, atuonyesha kanda ya video kabla na hata baada ya upasuaji huo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Chapisho la mtandao wa Twitter la Daktari lakdawala

Akitaja afya ya dadake kuwa mbaya.

Alisema kuwa: Anakabiliwa na upungufu wa oksijen katika mwili wake .Ni lazima avae kifaa cha oksijen kila mara, kuna mrija kutoka kwenye pua yake hadi katika tumbo lake kwa sababu hawezi kula vizuri kwa kutumia mdomo wake.

Lakini msemaji wa hositali hiyo ameambia BBC kwamba bi Abd El Aty alipimwa uzani tena siku ya Jumatatu na sasa ana uzani wa kilo 172.

Daktari Lakdawala naye alikana madai hayo katika chapisho lake la mtandao wa Twitter.

Eman Abdi aliugua kiharusi akiwa na umri wa miaka 11 na uzani wake ulimfanya kushindwa kuondoka nyumbani kwao kwa miaka 25.

Alisafirishwa kwa ndege hadi hospitali ya Saifee mjini Mumbai mnamo mwezi Januari ambapo alifanyiwa upasuaji wa kupunguza utumbo mnamo mwezi Machi na kundi moja la madaktari walioongozwa na Lakdawala.

Hospitali inasema kuwa sasa anaweza kutosha katika kiti cha magurudumo na kuketi kwa muda mrefu.

Hospitali hiyo ilitoa picha mpya za bi Abd El Aty kufuatia upasuaji huo wa kumpunguza uzani.

Ripoti zinasema kuwa bi Selim hafurahii kwa sababu mamlaka ya hopsitali hiyo inaamini kwamba matibabu ya bi Abdi El Aty yanakaribia kukamilika na kwamba hawezi kurudishwa nyumbani Alexandria hivi karibuni.

''Kuna visa kama hivi katika maeneo mengine duniani.Nchini Marekani na mataifa mengine watu waziti zaidi.Wamekwenda hospitalini kwa mwaka mmoja ama miwili ili kupunguza uzani na kuwa kawaida.Lakini baada ya mwezi moja au miwili madaktari wanasema naweza kumrudisha nyumbani dadangu.Niliwauliza kwa nini na bado ana uzani mkubwa na iwapo kitu chochote kitatokea nchini Misri, nitawezaje kumpeleka hospitali?

''Itakuwa vigumu na hakuna mtu atakayenisaidia Misri.Nilisema tafadhali ,tafadhali awachwe aendelee kuwa hospitali ili apunguze uzani'', alisema dadake.

Image caption Upasuaji wa Utumbo ili kupunguza zani

Upasuaji wa kupunguza utumbo ambao hujulikana kama upasuaji wa kupunguza uzani hutumika kama matibabu ya mwisho ya kutibu watu ambao ni wanene wa kupitia kiasi