Korea Kaskazini yafanya zoezi la kijeshi

Korea Kaskazini imefanya zoezi kubwa la kijeshi ambapo ufyatuaji wa risasi ulifanyika ili kuadhimisha miaka 85 tangu uzinduzi wa jeshi lake.
Image caption Korea Kaskazini imefanya zoezi kubwa la kijeshi ambapo ufyatuaji wa risasi ulifanyika ili kuadhimisha miaka 85 tangu uzinduzi wa jeshi lake.

Korea Kaskazini imefanya zoezi kubwa la kijeshi ambapo ufyatuaji wa risasi ulifanyika ili kuadhimisha miaka 85 tangu uzinduzi wa jeshi lake.

Mamlaka ya Korea Kusini imesema kuwa idadi kubwa ya vifaa vyake vya kijeshi vimepelekwa katika eneo la Wonsan kwa zoezi la kijeshi.

Korea Kusini pia imesema kuwa wanamaji wake wamekuwa wakifanya mazoezi ya pamoja na meli za kijeshi za Marekani.

Wajumbe kutoka Korea Kusini, Marekani na Japan wanafanya mazungumzo mjini Tokyo.

Mapema mjini Washington rais Trump alisema kuwa Korea Ksakzini ni tisho la ulimwengu.

Amewaalika maseneta wote 100 kwa mkutano katika ikulu ya Whitehouse siku ya Jumatano kuhusu hali ilivyo Korea Kaskazini.