Wanasayansi wagundua viwavi wanaokula plastiki

Wanasayansi wagundua viwavi wanaokula plastiki Haki miliki ya picha CÉSAR HERNÁNDEZ/CSIC
Image caption Wanasayansi wagundua viwavi wanaokula plastiki

Viwavi wanaokula plastiki huenda wakawa utatuzi wa uchafuzi wa mazingira unaofanywa na plastiki kulingana na wanasayansi.

Waafiti katika chuo kikuu cha Cambridge wamegundua kwamba buu la nondo huyo ambalo linakula nta pia linaweza kula plastiki.

Utafiti umebaini kwamba mdudu huyo anaweza kuharibu mshikamano wa kikemikali wa plastiki vilevile anavyokula nta ya nyuki.

Kila mwaka,takriban tani milioni 80 za plastiki huzalishwa duniani.

Plastiki hizo hutumika kutengeza mifuko ya plastiki inayotumika katika maduka ya jumla kubebea bidhaa na inaweza kuchukua muda mrefu kuoza.

Haki miliki ya picha CSIC COMMUNICATIONS DEPARTMENT
Image caption Viwavi wanaweza kuweka mashimo katika mifuko hiyo ya plastiki chini ya saa moja.

Hatahivyo viwavi wanaweza kuweka mashimo katika mifuko hiyo ya plastiki chini ya saa moja.

Daktari Paolo Bombeli ambaye ni mmoja ya watafiti anasema: Tutaanza na viwavi hao ,aliambia BBC.

''Tunahitaji kujua maelezo kuhusu vile viwavi hao wanavyofanya kazi.Tunahitaji kupata suluhu ili kuweza kupunguza plastiki''.