Mchungaji akana kuongoza kampeni ya kuchoma Biblia Uganda

Mtu akisoma kitabu cha Biblia Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtu akisoma kitabu cha Biblia

Mchungaji mmoja nchini Uganda amekana kuchoma vitabu vya biblia kulingana na kundi moja la kanisa la Pentecostal.

Kundi hilo la National Fellowship Of Born Again Pentecostal Churches of Uganda (NFBPC) linasema kuwa lilikutana na mchungaji Aloysious Bugingo siku ya Jumapili baada ya kushangazwa na ripoti kwamba alikuwa akiongozoia kampeni ya kuchoma biblia.

Kanda ya video ya hivi karibuni iliwekwa katika mtandao ikimuonyesha mchungaji huyo akishutumu biblia mpya.

Picha pia zimesambazwa za biblia zikichomwa, mchungaji huyo haonekani ndani yake.

Katika kanda hiyo ya video mchungaji huyo anaonekana akizungumza kwa mchanganyiko wa lugha za Kiingereza na Luganda akisema: Je mumeichunguza vizuri, imejaa mapepo, ndio inafaa kuchomwa. Je uliisoma hiyo? Ina mapepo ileteni....Watu kutoka kwa shirika la Biblia walitaka kuniita ili kuelezea.Lakini nimewaambia sio muhimu kunielezea.Waambie wale wanaoichapisha kurudisha vifungu vyake pale vinapohitajika, na waiandike vile inavyotakikana. iandikwe inavyohitajika. Kwa kweli sina haja ya mkutano wowote na mtu yeyote. Sihitaji! Iwapo ninafanya makosa.Niko tayari kwenda motoni.

Katika taarifa, Joshua Lwere wa NFBPC alisema kuwa alikana kuchoma biblia na kukubali kwamba utata kuhusu nakala za zamani za uhalisia wake unaweza kutatuliwa na bodi na wataalam pamoja na wasomi.

''Hivyobasi ninawaagiza wakristo na wasio wakristo kutochoma biblia.Toleo lolote lile la biblia unayomiliki tafadhali iheshimu kama neno la Mungu,licha ya tofauti yoyote ama tafsiri''.

Mchungaji Bugingo ambaye ni kiongozi wa jumba la ibada, anaishi mjini Kampala .Anaita mahala ambapo kanisa lake lipo Canaan.