Wizi wa mifugo utaangamizwa Kenya?
Huwezi kusikiliza tena

Mbinu mseto zinatumiwa kupatanisha jamii za wafugaji Kenya

Je, wizi wa mifugo utaangamizwa Kenya?

Wizi wa mifugo umekuwa tatizo sugu miongoni mwa jamii za wafugaji kaskazini magharibi mwa Kenya, hata baada ya juhudi za upatanisho ambazo zimekuwa zikiendeshwa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali pamoja na viongozi wa kijamii.

Mbinu mbalimbali za kutafuta amani zinatumiwa na Mashirika yasiokuwa ya serikali na jamii.

Hivi karibuni, visa vya wizi wa mifugo na uvamizi wa mashamba makubwa ya binafsi vimekuwa vikiripotiwa.

Anthony Irungu ana taarifa Zaidi kutoka kaunti ya Isiolo ambapo shirika la Nothern Rangelands Trust (NRT) linajihusisha na shughuli za kuhamasisha umuhimu wa amani.