Faru weupe wako hatarini Kenya

Maktaba Haki miliki ya picha AFP
Image caption Faru weupe

Faru wa mwisho mwenye jinisa ya kiume na mwenye umaarufu mkubwa duniani, mwenye rangi nyeupe, ajulikanaye kama faru mweupe wa Kaskazini amejiunga katika mpango wa kumbukumbu za Tinder, ikiwa ni sehemu ya harambee yenye juhudi za wahafidhina na wanaharakati wa wanyama nchini Kenya ambao wanajaribu kuokoa aina hiyo ya Faru adimu.

Juhudi za kukutana na wanyama wenye umri mkubwa wakiwemo faru hao wawili zimegonga mwamba. Wahafidhina wa masuala ya wanyama pori wametamka kwamba wanahitaji dola milioni kumi za Kimarekani kuendeleza kizazi hicho.

Faru hao weupe wa Kaskazini ndiyo faru pekee ambao wanaweza kuhimili kuishi porini katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Uchache wao umetokana na wawindaji haramu kuwaua kwa kasi. Faru hao wawili ambao ni manusura wanapewa ulinzi wa saa ishirini na nne.