Kiongozi wa upinzani Zambia kufikishwa mahakamani

Zambia
Maelezo ya picha,

Hakainde Hichilema Kiongozi wa upinzani nchini Zimbia ashtakiwa kwa uhaini

Kinara mkuu wa chama cha upinzani nchini Zambia, Hakainde Hichilema, anatazamiwa kufikishwa katika mahakama kuu nchini humo, kujibu mashtaka ya uhaini.

Hayo yameamuliwa na jaji wa mahakama kuu katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka.

Bw. Hichilema na chama chake wamekuwa wakiandika katika mtandao wa kijamii wa Tweeter kuhusiana na hatua hiyo.

Hichilema anatuhumiwa kwa kupanga njama za kuipindua serikali ya Rais Edgar Lungu.

Mwezi uliopita, alikamatwa baada ya msafara wake wa magari, ulipokataa kupisha ule wa Rais Lungu barabarani.

Licha ya kuwepo kwa juhudi za kidiplomasia kutanzua swala hilo, wanachama wa upinzani wanashinikiza hukumu hiyo ibatilishwe, kwani imechochewa kisiasa.

Hii sio mara ya kwanza kwa Hakainde Hichilema kukamatwa.

Mwezi Oktoba mwaka jana, mwanasiasa huyo alizuiliwa gerezani usiku kucha, baada ya kutuhumiwa kupanga mkutano wa kisiasa bila idhini, na kosa la uhaini baada ya kujaribu kuzuru gereza.