Marekani yaweka mtambo wa kulinda Korea Kusini

Terminal High Altitude Area Defense (THAAD) Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mtambo huo unatarajiwa kuzuia makombora yanayoilenga Korea Kusini

Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.

Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora, ambao hufahamika kitaalamu kama THAAD, kwa Kiingereza Terminal High Altitude Area Defense, kutokana na wasiwasi wa tishio kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia majaribio makombora.

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa an utakuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kumekuwepo na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na polisi eneo panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa mchezo wa gofu.

Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju

China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.

Rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.

THAAD ni nini?

  • Ni teknolojia ya kujilinda ya kutungua makombora ya masafa mafupi na wastani ambayo huyaharibu yanapokaribia kulipuka.
  • Hugonga kombora la kuliharibu
  • Ina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 200 na inaweza kurushwa juu hadi kilomita 150 angani
  • Marekani imewahi kuweka mitambo kama hiyo Guam na Hawaii kujilinda dhidi ya uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini
Image caption Mtambo huo hufanya kazi kwa kutungua makombora ya adui
Image caption Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii