Ugonjwa usiojulikana waua watu 8 Liberia

Sampuli za damu za waliofariki zinafanyiwa uchunguzi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sampuli za damu za waliofariki zinafanyiwa uchunguzi

Wizara ya afya nchini Liberia inasema kuwa inafanyia uchunguzi sampuli za damu kutoka kwa watu 8 ambao wamefariki kutokana ugonjwa usiojulikana katika kaunti ya Sineo kilomita 350 kusini mashariki mwa mji mkuu Monrovia.

Msemaji wa wizara ya afya Sorbor George, alisema kuwa jitihada za kuwaokoa wale walifariki zilishindwa,

Bwana George aliongeza kuwa watu wengine watano wanaoonyesha dalili za ugonjwa huo wamelazwa hopsitalini.

Redio ya taifa iliutaja kugonjwa huo kama usio wa kawaida.

Karibu watu 5000 walifariki nchini Liberia kutokana na ugonjwa wa ebola mwaka 2015 wakati utawala ulikosolewa kwa kutochukua hatua za haraka kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

Lakini hakuna ripoti ikiwa watu hao walifariki kutokana na Ebola na taarifa kutoka eneo hilo zinasema watu hawakuwa na dalili za na ugonjwa wa Ebola.

Barua iliyotumwa kwa wafanyakaziwote wa umoja wa mataifa nchini Liberia pia ilielezea vifo hivyo.

Barua hiyo ilisema kuwa 7 ya hao walifariki kati ya saa nane usiku na saa tano asubuhi siku Jumanne.

Vifo hivyo vinahusishwa na kisa cha siku ya Jumapili ambapo msichana wa umri wa miaka 11 ambaye alikuw na dalili za kuhara, kutabika na kuchanganyiwa akili alifariki.

Barua inasema kuwa waathiriwa wanaonekana kuhudhuria mazishi eneo moja.