Mwanamke anayetaka China kula wadudu

Mwanamke wa China anayefanya kampeni za kula wadudu ili kuimarisha tabia za kula nchini humo. Haki miliki ya picha RYAN LASH/TED
Image caption Mwanamke wa China anayefanya kampeni za kula wadudu ili kuimarisha tabia za kula nchini humo.

Mfanyibiashara mmoja wa Uchina anafanya kampeni za kula wadudu ili kuimarisha tabia za kula nchini humo.

Matilda Ho alizungumza katika mkutano wa Teknonoljia, utumbuizaji na mitindo kuhusu umuhimu wa kusambaza ujumbe wa chakula chenye afya.

Anaunga mkono vyakula ikiwemo vile vilivyo na protini kutoka kwa viwavi.

China ina tatizo la ukuwaji kutokana na kunenepe kupitia kiasi na ugonjwa wa kisukari.

''China ina asilimia 20 ya watu duniani lakini ni aslimia 7 pekee ya ardhi yake ilio na rutba'', alisema bi Ho.

Mtu mmoja kati ya raia wanne wa Uchina anaugua ugonjwa wa kisukari na mmoja kati ya watu wanne amenenepa kupita kiasi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wadudu kwa jina Silkworms anaofanya kampeni kwa Wachina kuwala

Bi Ho alianza kukabiliana na swala hilo kupitia soko la mtandao la wakulima ambalo sasa linatoa bidhaa 240 kutoka kwa walkulima 57.

Mtandao huo umepata wateja 40,000 tangu uzinduliwe miezi 18 iliopita.

''Nilitaka kutumia teknolojia ili kupunguza pengo lililopo kati ya wakulima na wanunuzi'', bi Ho aliambia BBC.

''Ni haki yako kujua kule chakula chako kinakotoka na kuwahamasisha wateja''.

Chakula hicho husambazwa kwa wateja kupitia magari ya kielektroniki na maboksi.