Rais Magufuli awaonya wanaotaka kuvunja muungano
Huwezi kusikiliza tena

Rais Magufuli awaonya wanaotaka kuvunja muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli ametoa tahadhari kwa yeyote yule atakayejaribu kuvunja muungano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar.

Onyo hilo amelitoa leo mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, yaliyofanyika mjini Dodoma.

Aidha Rais Magufuli amekiri kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana bado kuna changamoto mbalimbali zinazoukabili Muungano huo.