Mlipuko wakumba uwanja wa ndege Damascus

Mlipuko wakumba uwanja wa ndege wa Damascus Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mlipuko wakumba uwanja wa ndege wa Damascus

Mlipuko mkubwa umekumba eneo moja karibu na uwanja wa ndege wa Damascus kulingana na shirika la waangalizi wa haki za kibinaadamu nchini humo the Syrian Observatory for Human Rights.

Mlipuko huo uliokuwa mkubwa uliweza kusikika mjini Damscus, alisema Rami Abdel Rahman mkuu wa shirika hilo nchini Uingereza.

Uwanja huo wa ndege upo yapata kilomita 25 kusini mashariki mwa mji mkuu wa Syria.

Mlipuko huo ulifuatiwa kwa karibu na moto mkubwa.Hakuna habari zozote kuhusu majeraha.

Syria imekabiliwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tangu 2011.

Mzozo huo umewaua zaidi ya watu 320,000 na baada ya miaka sita hakuna suluhu ya kisiasa iliopatikana.