US: Mfumo wa kujilinda ''utamuamsha'' rais wa K. Kaskazini

Upelekaji wa mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini ulipingwa na waandamanaji Haki miliki ya picha AFP
Image caption Upelekaji wa mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora nchini Korea Kusini ulipingwa na waandamanaji

Mfumo wa kujilinda dhidi ya makombora wa Marekani unaowekwa nchini Korea Kusini utaanza kufanya kazi katika siku chache zijazo, jeshi la Marekani limesema.

Mfumo huo wa Thaad umetengezwa kuilinda Korea Kusini na majeshi ya Marekani yaliopiga kambi nchini humo dhidi ya vitisho vya Korea Kaskazini.

Vifaa vya mfumo huo vilipelekwa katika taifa hilo siku ya Jumatano, Admirali Harry Harris ambaye ni ni kamanda wa eneo la Pacific alisema kuwa Thaada itaanza kufanya kazi katika siku chache zijazo ili kuiinda Korea Kusini dhidi ya vitisho vya jirani yake Korea kaskazini.

Amesema kuwa mfumo huo unalenga ''kumfungua macho'' rais Kim Jong un na ''sio kumuangusha''.

Image caption Makombora yanayomilikiwa na Korea Kaskazini

Wizara ya ulinzi baadaye ilithibitisha kwamba mfumo huo utaanza kufanya kazi hivi karibuni.

Msemaji amesema kuwa uwepo wa vifaa unamaanisha kwamba Korea Kusini na Marekani zina uwezo kukabiliana na uchochezi wa Korea Kaskazini.