Kisiwa kilichotumiwa kuwaadhibu wasichana walioshika mimba nje ya ndoa

Kisiwa cha adhabu nchini Uganda kilitumika kuwaadhibu wasichana walioshika mimba nje ya ndoa
Image caption Kisiwa cha adhabu nchini Uganda kilitumika kuwaadhibu wasichana walioshika mimba nje ya ndoa

Wasichana waliopata mimba bila ya kuolewa walionekana kuleta aibu katika familia katika maeneo ya Uganda, hivyobasi walikuwa wakichukuliwa hadi katika kisiwa kidigo na kuwachwa kufa.

''Waliokuwa na bahati waliokolewa na mmoja wao angali hai''.

''Wakati wazazi walipogundua kwamba mimi ni mjamzito waliniweka katika mashua na kunipeleka katika kisiwa cha Akampene''.

''Niliishi huko bila chakula ama hata maji kwa siku nne'', anasema Mauda Kyitaragabirwe, aliyekuwa na umri wa miaka 12 wakati huo.

''Nakumbuka nikihisi njaa na baridi.Karibia nifariki.Siku ya tano mvuvi mmoja alikuja na kusema atanichukua na kumpelea nyumbani.Nilikuwa na wasiwasi''.

Image caption Hapa ndio katika eneo ambalo Bi Kyitaragabirwe aipelekwa na kuwachwa

Nilimuuliza iwapo alikuwa ananidanganya na kwamba alitaka kunitupa katika maji.lakini alisema: hapana. Nakuchukua ili kukufanya mke wangu.

''Kwa hivyo alinileta hapa'', akanionyesha nyumba ambayo anaishi yeye na mumewe pekee.

Anaishi katika kijiji cha Kashungyera, ambapo kiko dakika 10 ukivuka ziwa Bunyoni kutoka kisiwa cha adhabu.

Kwanza bi Kyitaragabirwe hakujua namna ya kunisalimia hadi pale Tyson Ndamwesiga, mjukuu wake alipomwambia kwamba ninazungumza lugha ya Rukiga.

Alinishika mkono kutoka katika kisukusuku wanavyofanya watu wa Bakiga kwa mtu waliyekutana naye baada ya miaka mingi.

Bi Kyitaragabirwe anakadiria kwamba ana umri wa miaka 80 lakini familia yake inaamini kwamba ana miaka zaidi.

Image caption Kisiwa cha adhabu nchini Uganda

Alizaliwa wakati vyeti vya kuzaliwa vilikuwa nadra katika eneo hilko la Uganda kwa hivyo hana uhakika kuhusu miaka yake.

Alikuwa akimiliki cheti cha kupigia kura kabla ya uhuru wa Uganda mwaka 1962.

''Hiyo ndio tuliyokuwa tukitumia kuhesabu kutoka nyuma tunadhani ana takriban miaka 106'',anasema Ndamwesiga.

Katika jamii ya Bakiga, mwanamke kijana anafaa kushika mimba baada ya kuolewa.

Kuoa msichana aliye bikra kulimaanisha kupokea mahari iliolipwa kwa kutumia ng'ombe.

Mwanamke ambaye ana mimba na hajaolewa alionekana kutoleta aibu pekee bali pia aliipokonya mali familia.

Image caption Bi Kyitaragabirwe

Familia zilikuwa zikiondoa aibu hiyo kwa kuwatupa wasichana walio na mimba katika kisiwa cha adhabu, na kuwawacha wakifa.

Kutokana na umbali wa eneo hilo tabia hiyo iliendelea hata baada ya wamishenari na wakoloni kuwasili nchini Uganda katika karne ya 19 na kuisitisha.

Watu wengi wakati huo hususan wasichana hawakujua kuogelea.

Kwa hivyo iwapo mtu angepelekwa katika kisiwa hicho alikuwa na fursa mbili kuruka katika maji na kufariki ama asubiri auawa kutokana na baridi na njaa.

Nilimuuliza Kyitaragabirwe iwapo aliogopa,na alinijibu, ukuwa kama umri wa miaka 12 halafu uchukuliwe nyumbani kwenu hadi katika kisiwa ambapo hakuna mtu anayeishi katikati ya Ziwa usingeogopa?