Papa Francis awasili nchini Misri

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis awasili Misri kwa ziara ya kidini Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis awasili Misri kwa ziara ya kidini

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amewasili nchini Misri kwa ziara fupi inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidini na ulimwengu wa Kiislamu.

Ziara hiyo inajiri wakati ambapo kuna ongezeko la mauaji ya Wakristo waliopo katika mashariki ya kati hususan wale wa jamii ya kanisa la Coptic.

Mapema mwezi huu kundi la Islamic state lilikiri kutekeleza shambulio la mabomu ya makanisa mawili ya Coptic.

Papa Francis atakutana na rais wa Misri na kutoa hotuba kuhusu amani katika chuo kikuu cha Al-Azhar, taasisi ya masomo ya Kiislamu miongoni mwa madheheu ya Sunni.

Mlipuko waua watu wengi kanisani Cairo, Misri

Milipuko yawaua watu 36 kanisani nchini Misri

Papa Francis aongoza maelfu kwa ibada St Peter's Square

Ataonyesha umoja wake na mwenzake wa kanisa hilo Tawadrod II akijumuika naye katika kanisa lililoshambuliwa mnamo mwezi Disemba.

Uhusiano kati ya Vatican na Waislamu wengi ulishuka 2006 wakati mtangulizi wa Papa Francis Benedict alipoonekana akihusisha Uislamu na ghasia.

Image caption Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis awasili Misri kwa ziara ya kidini