Maiti yachoma chumba cha kuchomea wafu Marekani

Chumba cha kuchomea mfu huko Ohio Marekani

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Chumba cha kuchomea mfu huko Ohio Marekani

Chumba cha kuchomea maiti katika jimbo la Ohio nchini Marekani kilichomeka wakati kilipokuwa kikitumika kuchoma mwili wa mfu aliyenenepa kupita kiasi kulingana na mmiliki wa chumba hicho.

Don Catchen alisema kuwa maiti hiyo ilisababisha moto uliochoma chumba hicho katika mji wa Cincinati.

Mafuta yaliokuwa katika mwili huo yalichomeka katika viwango vya juu vya joto na kusababisha moto huo kulingana na afisa mkuu wa zima moto.

Hatahivyo hakuna eneo jingine la chumba hicho lililochomeka kulingana na Catchen.

Moto huo hatahivyo ulidhibitiwa katika eneo la kutengeza magari ambapo chumba hicho cha kuchomea maiti kipo,aliambia BBC.

Chanzo cha picha, HILLSIDE CHAPEL

Maelezo ya picha,

Chumba hicho kipo katika mji wa Cincinati.

''Mfanyikazi wangu alikuwa katika hatua ya kuchoma mwili mmoja wa mtu aliyenenepa kupitia kiasi na moto ukawa mkubwa zaidi ya kiwango kinachohitajika''.

"Mojawapo ya makasha ya kuchoma mili lilichomeka na ni hilo ndio lililochomeka pekee.Hakuna miili mingine ilioharibika katika moto huo'',alisema.