Korea Kaskazini yalaumiwa kwa kuonyesha silaha bandia

Maonyesho ya kijeshi ya Korea Kaskazini yalionyeshwa kote duniani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maonyesho ya kijeshi ya Korea Kaskazini yalionyeshwa kote duniani

Korea kaskazini inaluamiwa kwa kuonyesha silaha bandia katika maonyesho ya hivi majuzi ya ubabe wake wa kijeshi.

Afisa wa zamani wa masuala ya ujasusi anasemna baadhi ya bunduki na makombora yaliyotumiwa kwenye maonyesho hayo yalikuw bandia.

Michael Pregent alikiambia kituo cha runinga cha Fox kuwa baadhi ya bunduki zilizokuwa kwenye maonyesho hayo zilikuwa ni za kujekesha

Lakini maonyesho kama hayo kuonyesha ubabe wa kijeshi yametumiwa kwa miongo kadha.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maonyesho ya kijeshi mjini Pyongyang

Kwa sasa msukosuko ni mkubwa kati ya Marekani na Korea Kaskazini.

Hii ni baada ya rais wa Marekani kuapa kuwa ni lazima atakabiliana na tisho la Korea Kaskazini.

"Sio kuwa Korea kaskazini inafikiri kuwa itashinda Marekani lakini kile itafanya ikiwa itashambuliwa," bwa Pregent alisema.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Wanajeshi wa Korea Kaskazini

Historia ya silaha bandia

Haki miliki ya picha National Archives
Image caption Vifaru bandia vilitumiwa na Uingereza wakati wa vita vya pili vya dunia kuonyesha ubabe wa kijeshi

Silaha hizi bandia zilitengenezwa kukwepa mashambulizi ya angani na kuwachanganya marubani ya jeshi kushambulia vifaru bandia baada ya vifaru halali

Wasani ya jeshi la Ufaransa nao walichora mito bandia na mitaro ili kuwachanganya marubani wa ndege za vita.

Ujanja kama huo pia ulitumiwa wakati wa vita vya pili vya Dunia

Haki miliki ya picha National Archives
Image caption Vifaru bandia
Haki miliki ya picha National Archives
Image caption Mruka na mwavuli bandia wakati wa vita vya pili vya dunia

Miongo kadha kabla miti ilitumika kupigana katika vita vya wenyewe nchini Marekani

Miti hii ilipakwa rangi hadi kifanana na silaha ya kurusha makombora.

Lengo lilikuwa ni kuwachanganya maadui kuhusu ni wapi kulikuwa na adui.

Haki miliki ya picha Corbis/Getty Images
Image caption Bunduki bandia za miti

Aina hii ya silaha bandia zilitumika karne za 18 na 19

Picha hii inaonyesha wanajeshi wa Ujerumani wakikimbia ndani ya vifaru bandia miaka ya 1920

Haki miliki ya picha Getty Images/Hulton Archive
Image caption Wanajeshi wa Ujerumani wakikimbia ndani ya vifaru bandia