Wanariadha wa Kenya wapatwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu

Wanariadha wa kenya wapatwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wanariadha wa kenya wapatwa na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu

BBC imefahamu kuwa chama cha riadha cha kenya kumepata ripoti inayoonyesha kuwa wanariadha wawili wa Kenya wa mbio za masafa marefu, ambao bado hawajatajwa wamepatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu za mwili.

Chama hicho kinachelewa kutaja majina ya wanariadha hao kuzuia kuharibu sherehe za kumkaribisha mwanariadha Mary Keitany ambaye alishinda mbio za London Marathon wiki iliyopita na kuvunja rekodi ya dunia.

Wiki tatu zilizpita mwanariadha mwingine mkenya na mshindi wa zamani wa mbio za London Marathon Jemima Sumgong, alipigwa marufuku kwa kupatikana kutumia dawa za kuongeza nguvu za mwili.

Baadhi ya wanariadha maarufu wa Kenya wana hofu kuwa sakata hizo huenda zikachafua mafanikio yao na wametaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahusika.