Mtoto aliyezaliwa na miguu 3 afanyiwa upasuaji Australia

Mtoto wa miaka mitatu aliyezaliwa na miguu mitatu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mtoto wa miaka mitatu aliyezaliwa na miguu mitatu

Mtoto mmoja nchini Bangladesh aliyezaliwa akiwa na miguu mitatu amefanyiwa upasuaji nchini Australia na sasa anarudishwa nyumbani

Choity Khatun ambaye ana miaka mitatu alizaliwa na ulemavu huo ambapo mguu huo ulikuwa umemea katika mfupa wake wa kiuno.

Wapasuaji wa Australia walitumia mwezi mmoja wakifanya kazi ya kuuondoa mguu huo na kurekebisha eneo lake la mfupa wa kiunoni.

Mtoto huyo alipelekwa Australia kutoka kijijini kwao huko Bangladesh na shirika moja la hisani Children first Foundation.

Daktari Chris Kimber ,kiongozi wa upasuaji katika hospitali ya Monash huko Victoria alisema kuwa kesi ya Choite ilikuwa isio ya kawaida na kwamba upasuaji huo ulikuwa mgumu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Picha ya X ray ya Mtoto mmoja nchini Bangladesh aliyezaliwa akiwa na miguu mitatu

''Upasuaji hutegemea mtu anayefanyiwa na lazima utumie muda mwingi kuchanganua ni nini kilichopo na baadaye upange mpango unaoshirikisha hayo yote'', aliambia kituo cha habari cha Australia Broadcasting Cooperation.

Kundi hilo la madaktari wa Australia pia lilikuwa limefanya majadiliano kuhusu upasuaji huo

Lilijadiliana iwapo upasuaji huo ulihitajika na kwamba ungemfaidi kabla ya mtoto huyo kupelekwa Australia.