Afrika kwa Picha: 21-27 April 2017

Mkusanyiko wa picha bora zaidi kutoka Afrika na kuhusu Waafrika pande mbalimbali duniani wiki hii.

Haki miliki ya picha Tamasin Ford
Image caption Masapeur (wapenda mavazi ya madaha) kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Ivory Coast walikusanyika Jumanne kumkumbuka gwiji wa muziki Papa Wemba aliyefariki akitumbuiza katika tamasha la muziki la Femua mjini Abidjan mwaka mmoja uliopita...
Haki miliki ya picha Tamasin Ford
Image caption Alikuwa mfalme wa Masapeur na mwanzilishi wa "La Sape" (Chama cha watu wapenda mavazi ya madaha)...
Haki miliki ya picha Tamasin Ford
Image caption Masapeurs huwa ni lazima wavalie nadhifu, wajipambe kwa vito na lazima wawe na manukato yanayonukia vyema.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jumatano, mwanamke alikuwa anauza nguo za ndani za mutumba (nguo ambazo tayari zimeshatumika) mjini Lagos, Nigeria.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Siku iyo hiyo, mwanamume anasukuma toroli katika barabara moja mtaa wa Okepopo, Lagos.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jumamosi, mwanamke anaketi ndani ya duka la kuuza vitu vya kumbukumbu vya Kikristo kabla ya ziara ya Papa Francis mjini Cairo
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan (Kushoto) akiwa na Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed wakikagua gwaride la heshima mjini Ankara, Uturuki.
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mchukuzi akisafirisha mapipa katika mtaa mmoja viungani mwa jiji la Nairobi, kenya
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mfuasi wa chama cha Orange Democratic Movement akiwa katika mkutano wa siasa wa muungano wa upinzani ambapo Raila Odinga alitangazwa kuwa mgombea wa muungano wa huo.

Picha kwa hisani ya AFP, EPA, Getty Images na Reuters

Mada zinazohusiana