Trump: Ninakosa maisha yangu ya zamani

Trump alisema aliyapenda maisha yake ya zamani kwa sababu ni mengi yalikuwa yakifanyika, Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Trump alisema aliyapenda maisha yake ya zamani kwa sababu ni mengi yalikuwa yakifanyika

Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akizungumza kuhusu maisha ya awali kabla ya kuwa rais na kueleza jinsi wajibu wake huo mpya katika Ikulu ya White House ni ngumu.

Trump alisema aliyapenda maisha yake ya zamani kwa sababu ni mengi yalikuwa yakifanyika, alipozungumza na shirika la habari la Reuters akiwa White House.

"Hii ni kazi nyingi zaidi kuliko ya maisha yangu ya awali, alisema. "Nilifikiri itakuwa rahisi."

Matamshi yake Trump ya kuwa rais yamejadiliwa katika mitandao ya kijamii, wengi wakielezea mshangao wao.

"Ninakosa maisha yangu ya awali," alisema Trump.