Wladmir Klitschko kuzipiga na Anthony Joshua

Anthony Joshua kushoto dhidi ya Wladmir Klitschko
Image caption Anthony Joshua kushoto dhidi ya Wladmir Klitschko

Takriban watu 90,000 wataujaza uwanja wa Wembley siku ya Jumamosi kuona pigano la uzani mzito duniani kati ya bingwa wa ukanda wa IBF Anthony Joshua wa Uingereza anayejaribu kutaka kuongeza ukanda mwengine wa WBA wakati atakapokabiliana na aliyekuwa bingwa duniani Wladmir Klitschko.

Mabondia hao wawili wamewachana na umri wa miaka 14 huku raia huyo wa Uingereza akiwa na umri wa miaka 27 dhidi ya bondia ambaye alimsaidia kama mpiganaji mwenza wakati wa mazoezi.

lakini ni Joshua ambaye anaonekana kuwa bondia mwenye uwezo mkubwa.

Image caption Anthony Joshua kulia akimpiga makonde mazito mpinzani wake katika pigano la awali.

Je anaweza kulivaa taji hilo,kitengo cha michezo cha BBC walifanya mahojiano na mabondia tofauti,akiwemo bingwa wa zamani wa uzani huo kutoka Uingereza aliyefanikiwa kumshinda Klitscko Lenox Lewis .

''Nadhani ni wakati muhimu kwa Joshua kuuonyesha ulimwengu kwamba sasa amekomaa na hususan kwa sababu Klitschko anataka kulipiza baada ya kushindwa na Tyson Fury.

"kutokana na umri wa Klitscko hana nguvu tena za miguu, nguvu alizokuwa nazo zimepungua kuna maswala mengi tofauti ambayo yanamuathiri kimaisha.

Image caption Joshua kushoto na Klitscko kulia

"Ninaamini Joshua amejiandaa .Je anataka kuwa bingwa wa dunia? Ndio kabisa'',alisema Fury