Mmarekani aliyehukumiwa kwa kuipeleleza China arejea nyumbani

Sandy Phan Gillis, aliwasili Los Angales, ambapo alikaribishwa na mumewe. Haki miliki ya picha SAVESANDY.ORG
Image caption Sandy Phan Gillis, aliwasili Los Angales, ambapo alikaribishwa na mumewe.

Raia wa Marekani aliyehukumiwa kwa madai ya kuwa jasusi nchini China amerejea Marekani.

Sandy Phan Gillis, aliwasili Los Angales, ambapo alikaribishwa na mumewe.

Mumewe amekuwa akiongoza kampeni ya kutaka mkewe aachiwe huru kwa miaka miwili.

Mwanamke huyo mfanyibiashara alitiwa mbaroni wakati akijaribu kuondoka China, baada ya mkutano wa wajumbe wa biashara kutoka Houston Texas.

Mapema wiki hii, mahakama moja ya Uchina ilimhukumu kifungo cha miaka 3 na nusu gerezani , na vilevile ikaagiza arejeshwe mahakamani.