Baba mkwe wa El Chapo Guzman afungwa miaka 10

Baba mkwe wa El Chapo Guzman ahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kuingiza mihadarati Marekani
Image caption Baba mkwe wa El Chapo Guzman ahukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kuingiza mihadarati Marekani

Baba mkwe wa mlanguzi mkubwa wa dawa za kulevya , Joaquin Guzman, amehukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani kwa kupenyeza bangi nchini Marekani.

Ines Coronel Barreras alipatikana na makosa katika mahakama moja ya Mexico, baada ya polisi kutwaa magari silaha na zaidi ya kilo 250 za bangi.

Marekani ilimwekea vikwazo miaka minne iliyopita, na kusema kwamba ni mojawepo wa vigogo wa genge la Sinaloa.