Uturuki yaifunga tovuti ya Wikipedia

Tovuti ya Wikipeadia iliofungwa nchini Uturuki Haki miliki ya picha GETTY IMAGES/PETERMACDIARMID
Image caption Tovuti ya Wikipeadia iliofungwa nchini Uturuki

Uturuki imefunga tovuti ya maelezo ya Wikipedia nchini humo.

Waliojaribu kufikia mtandao wamepata ujumbe kwamba seva yake haifanyi kazi.

Idara ya mawasiliano imesema kwamba hatua mwafaka imechukuliwa kutatua tatizo hilo, japo haikutoa sababu yoyote ya mtandao huo kufungwa.

Tovuti zingine zinafanya kazi kama kawaida.

Uturuki imekuwa ikifunga mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter wakati wa maandamano makubwa ama mashambulizi ya kigaidi.