Anthony Joshua amwangusha Wladimir Klitschko

Bondia wa Uingereza Anthony Joshua amemwangusha Wladimir Klitschko wa Ukraine na kutawazwa bingwa wa dunia kitengo cha uzani mzito. Haki miliki ya picha PA
Image caption Bondia wa Uingereza Anthony Joshua amemwangusha Wladimir Klitschko wa Ukraine na kutawazwa bingwa wa dunia kitengo cha uzani mzito.

Bondia wa Uingereza Anthony Joshua amemwangusha Wladimir Klitschko wa Ukraine na kutawazwa bingwa wa dunia kitengo cha uzani mzito.

Mashabiki wa ndondi walishuhudia pigano la kukata na shoka ambapo, Joshua alimwangusha Wladimir katika raundi ya tano, na kwa mara ya kwanza katika taaluma yake, Joshua akaangushwa katika raundi ya 6

Joshua alinusa ushindi, baada ya kupata upenyu na kurusha ngumi ya kushtukiza ya mtunguo, iliyompa nafasi ya kumwangusha wladamir kwa msururu wa ngumi.

Pigano hilo lililoshuhudiwa na zaidi ya watu 90,000 katika uwanja wa Wembley mjini London, lilisimamishwa katika raundi ya 11 baada ya Joshua kumzidi nguvu Wladimir na kumuangusha.

Uwanja wa Wembley ulijawa kelele na shangwe wakati mwamuzi alisema Wladamir amezidiwa kabisa.

Joshua, ambaye ana umri wa miaka 27, ameshinda mechi zote 18 za awali kwa pigo la ushindi ama KO.

Pigano la jana lilikuwa la 19.