Marekani kugharamia mtambo ya kujikinga Korea Kusini

Marekani kugharamia mtambo ya kujikinga Korea Kusini Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Marekani kugharamia mtambo ya kujikinga Korea Kusini

Korea kusini inasema kuwa Marekani imekubali kulipa dola bilioni moja za kujenga kinga ya dhidi ya makombora ya Korea Kaskazini.

Awali rais Trump alikuwa amesema Korea kusini itagharamia ujenzi huo.

Maafikiano hayo yanajiri baada ya washauri wa maswala ya usalama wa mataifa hayo mawili kuzungumza kwa njia ya simu.

Ngao hiyo maalum ambayo inajengwa kwa sasa inalenga kudungua makombora yote yanayofyatuliwa kutoka Korea kaskazini.

Marekani imekubali kufadhili mradi huo kifedha huku korea kusini ikitakiwa kutoa ardhi.

Image caption Namna mfumo wa ulinzi wa THAAD unavyofanya kazi