Mwanzilishi wa Facebook aitembelea kwa ghafla familia moja Ohio

Mwanzilishi wa Facebook aitembelea kwa ghafla familia moja Ohio Haki miliki ya picha Mark Zuckerberg/Twitter
Image caption Mwanzilishi wa Facebook aitembelea kwa ghafla familia moja Ohio

Familia moja nchini Marekani imeeleza ilivyohisi wakati ilipata taarifa kwamba mwanzilishi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg angewatembelea kwa chakula cha jioni.

Familia hiyo ya Moore , eneo la Newton Falls, inasema walijua utambulisho wa mgeni wao dakika 20 kabla ya kuwasili ijumaa.

Bwana Zuckerberg anazuru majimbo yote 50 ya Marekani na amewataka wafanyikazi wake kutafuta wanachama wa Democrat waliompigia kura rais Donald Trump.

Anakisiwa kuwa na mpango wa kuwania urais wa Marekani.

Familia hiyo inasema bwana Zuckerberg alikuwa mtu mtulivu sana.