Mkurungenzi wa runinga ya Iran auawa Uturuki

Saeed Karimian alikuwa ndani ya gari pamoja na mshirika wake wa kibiashara Haki miliki ya picha SAEED KARIMIAN
Image caption Saeed Karimian alikuwa ndani ya gari pamoja na mshirika wake wa kibiashara

Mkurugenzi mkuu wa kampuni moja ya runinga ya Iran ameuwawa kwa kupigwa risasi akiwa mji mkuu wa Uturuki, Istanbul.

Saeed Karimian alikuwa ndani ya gari pamoja na mshirika wake wa kibiashara wakati watu waliokuwa na bunduki huku wakijifunika nyuso zao walishambulia gari lao.

Wote wawili waliuawa.

Runinga ya bwana Karimian, Gem TV, huwa inapeperusha vipindi vya mataifa ya magharibi na mataifa mengine kwa lugha ya kipersia.

Amekuwa akishutumiwa kwamba anaeneza taarifa za kupotosha dhidi ya Iran, huku mwanahabari wa BBC akisema kuna baadhi ya watu wanaosema kwamba aliuwawa na maafisa wa iran.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Runinga ya bwana Karimian, Gem TV, huwa inapeperusha vipindi vya mataifa ya magharibi kwa lugha ya kipersia.