Mpanda milima maarufu duniani afariki Everest

Ueli Steck ambaye alikuwa akiitwa Mashini ya Uswiswi, alikufa kwenye ajali akipanga mlima Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ueli Steck ambaye alikuwa akiitwa Mashini ya Uswiswi, alikufa kwenye ajali akipanga mlima

Mmoja wa wapanda milima maarufu zaidi duniani Ueli Steck, amefariki katika Mlima wa Everest.

Steck ambaye alikuwa akiitwa Mashini ya Uswiswi, alifariki kwenye ajali, alipokuwa akijaribu kujizoesha kupanda mlima huo kwa kupita njia mpya na bila ya kutumia gesi ya oxygen.

Steck, alikuwa na umri wa miaka 40, na ameshinda tuzo kadha huku akijulikana kwa kukwea milima kwa kasi.

Mwili wake umetolewa mlima Everest na kupelekwa mji mkuu wa Nepal, Kathmandu.

Ueli Steck aliweka reko mpya wa kukwea milima kwa kasi na kutumia njia mpya.

Pia alichangia katika mchezo huo kupata mashabiki wapya kutokana na filamu kumhusu zilizotengezwa.

Mwaka 2015 alipanda moja ya kuta maarufu zaidi duniani unaofahamika kama North Face of the Eige, kwa muda wa saa 2 na dakika 47, jaribio lililowachukua watangulizi wake siku kadha kukamilisha.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ueli Steck amefanikiwa kupanga mlima Everest awali bila hewa ya oxygen