Watumwa wa jamii ya Yazidi waokolewa Iraq

Wayazidi 36 walipelekwa Dohuk Kaskazini mwa Iraq Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wayazidi 36 walipelekwa Dohuk Kaskazini mwa Iraq

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq, inasema kuwa watu 36 wa kabila la Yazidi, waliotekwa kama watumwa na kundi la Islamic State, wameokolewa wakiwemo wanawake na watoto.

Wanaripotiwa kuwa kizuizini kwa karibu miaka mitatu.

Islamic State iliwauwa na kuwateka watu wengi wa Yazidi, ambao ni wa dini tofauti, wakati IS iliteka eneo la kaskazini mwa Iraq, mwaka 2014.

Wakurdi wa Peshmerga walidhibiti eneo hilo mwaka 2015 lakini Wayazidi wengi walikiliwa na Islamic State maeneo mengine wakati kundi hilo lilidhibiti sehemu kubwa za Kaskazini mwa Iraq.

Watu hao 36 walifika mji wa Dobuk siku mbili zilizopita ambapo walipewa hifadhi kwenye vituo vya Umoja wa Mataifa

Wanajumuishwa na familia zao huko na kupewa mahitaji ikiwemo nguo na madawa pamoja na ushauri wa kisaikolojia.

Umoja wa mataifa unaamini kuwa hadi wanawake na wasichana 1500 bado wanashikiliwa na huenda wanakumbwa na dhuluma za kingono.