Matteo Renzi arejea katika siasa za Italia

Matteo Renzi amekuwa waziri mkuu wa Italia tokea mwaka 2014-2016
Image caption Matteo Renzi amekuwa waziri mkuu wa Italia tokea mwaka 2014-2016

Waziri mkuu wa zamani wa Italia Matteo Renzi, anajaribu kurudi katika siasa kwa mara nyingine kutafuta uongozi katika chama cha Democratic Party.

Taarifa kutoka vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa ameshinda kwa zaidi ya asilimia 70 ya kura dhidi ya wapinzani wake ambao ni waziri wa sheria Andrea Orlando na mwanasiasa mkongwe Michele Emiliano.

Matokeo rasmi yanatarajiwa baadae.

Renzi alijiuzulu kama waziri mkuu na baadae kiongozi wa chama chake baada ya kushindwa kufanikisha mchakato wa mabadiliko ya katika mwezi Disemba.