Wabunge Marekani wakubaliana kuhusu bajeti

Wabunge wanatarajiwa kuipigia kura bajeti hiyo siku chache zinazokuja. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wabunge wanatarajiwa kuipigia kura bajeti hiyo siku chache zinazokuja.

Wapatanishi wa Congress nchini Marekani wameafikia makubaliano kuhusu mswada wa matumizi ya serikali ya hadi Septemba 30 mwaka huu.

Matumizi hayo yameongeza bajeti ya jeshi lakini hayajajumuisha ufadhili wa ujenzi wa ukuta uliopendekezwa na Trump kwenye mpaka wa Mexico.

Makubaliano hayo ya dola bilioni moja yanahitaji kuidhinishwa na wabunge.

Siku ya Ijumaa bunge la Congress lilidhinisha mswada wa matumizi ambayo yalizuia shughuli za serikali kukwama siku wa Ijumaa.

Wabunge wanatarajiwa kuipigia kura bajeti hiyo siku chache zinazokuja.

Ikiwa hatua hiyo haingechukuliwa mbuga za kitaiafa zingefungwa na wafanyakazi wa serikali kuachishwa kazi.

Kukwama kwa shughuli za serikali mara ya mwisho kulitokea mwaka 2013 kwa muda wa siku 17.

Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa hatua hiyo inampa Rais Donald Trump nyongeza ya matumizi ya jeshi ya dola bilioni 12.5 na nyingine ya dola bilioni 1.5 kwa usalama wa mipaka.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hatua hiyo inampa Rais Donald Trump nyongeza ya matumizi ya jeshi ya dola bilioni 12.5

Mji wa New York utapokea dola miioni 68 zaidi kwa usalama na kwa gharama ya kumlinda Rais Trump na familia yake.

Makubaliano hayo pia yanawapa wachimba mkaa wa mawe dola 1.3 kama marupurupu ya kiafya.

Mapema Rais Trump alikuwa amekabiliwa na shinikizo za wanademocrat wakati wa kutomtaka asijumuishe ufadhili wa ukuta kati ya Mareakni na Mexico.

Mada zinazohusiana