Binti mfalme wa Uingereza kutimiza miaka miwili

Princess Charlotte Haki miliki ya picha HRH THE DUCHESS OF CAMBRIDGE
Image caption Princess Charlotte

Picha ya binti mfalme Charlotte imetolewa na Kensington Palace kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa anapotimia umri wa miaka miwili siku ya Jumanne.

Picha hiyo aliyochukuliwa na mama yake, inamuonyesha Charlotte nyumbani mwa familia.

Familia ilitoa picha ya Charlotte sawa na hiyo mwaka uliopita alipotimia umri wa mwaka mmoja.

Kensington Palace ilisema kuwa kila mmoja anafurahia picha hiyo vile wao wenyewe wanavyoifurahia.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Alipigwa picha mara ya kwanza akitolewa St Mary's Hospital, na wazazi wake

Familia inatarajiwa kumuandalia karamu binti mfalme huyo.

Familia huzuia binti mfalme huyo kuonekana kwa umma lakini alipigwa picha wakati wa ibada ya krismasi katika kijiji cha Bucklebury.

Pia alionekana wakati familia ilifanya ziara nchini Canada ambapo alionekana mara kadha ikiwemo waki wa karamu ya watoto huko Victoria

Haki miliki ya picha HRH THE DUCHESS OF CAMBRIDGE
Image caption Prince George na Princes Charlotte
Haki miliki ya picha HRH THE DUCHESS OF CAMBRIDGE
Image caption Princess Charlotte
Haki miliki ya picha HRH THE DUCHESS OF CAMBRIDGE
Image caption Princess Charlotte
Haki miliki ya picha PA
Image caption Familia huzuia binti mfalme huyo kuonekana kwa umma
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Princcess Charlotte akiwa na mama yake