Kenyatta aongeza mshahara wa chini Kenya

Rais Kenyatta amesema kuwa hatua za kuboresha uchumia ili kuwawezesha wakenya kuishi maisha mema zinaendelea. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Kenyatta amesema kuwa hatua za kuboresha uchumia ili kuwawezesha wakenya kuishi maisha mema zinaendelea.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza nyongeza ya mshahara wa chini zaidi mfanyakazi anastahili kulipwa kwa asilimia 18.

Rais Kenyatta alitangaza hilo wakati wa sherehe za kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani iliyoandaliwa katika bustahi ya Uhuru mjini Nairobi

Hadi shilingi 100,000 za marupurupu na malipo ya kufanya kazi saa za ziada hazitatoswa kodi kama njia ya kuwapunguzia wakenya gharama ya kupanda kwa maisha.

Nao mshahara ulio chini ya shilingi 13,475 hautatoswa kodi.

Rais Kenyatta amesema kuwa hatua za kuboresha uchumia ili kuwawezesha wakenya kuishi maisha mema zinaendelea.

Amesema kuwa jitihada za sasa za ujenzi wa barabara, kuondoa vizuizi vya kufanya biashara na elimu bora ni baadhi ya hatua.

Image caption Kenyatta amesema shilingi bilioni 40 zimedhinishwa kwa ujenzi wa mji wa kiteknolojia wa konza

Rais amewataka waajiri kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanahudumu katika mazingira salama na kuongeza kwa serikali itaanzisha zoezi la kukagua usalama katika maeneo ya kazi.

Huku Kenya ikielekea kwenye uchaguzi mkuu rais Kenyatta amewataka wakenya kutojihusisha na ghasia akisema kuwa amani ndicho kigezo cha maendeleo ya nchi.

Kenyatta amesema shilingi bilioni 40 zimedhinishwa kwa ujenzi wa mji wa kiteknolojia wa konza. Amesema ujenzi wa mji huo utabuni nafasi za ajira 16,000 wakati ukijengwa na zingine zaidi ya 200,000 utakapokamilika kujengwa.

Rais Kenyatta pia amewashauri wakenya kufanya kazi na mashirika yaliyothibitishwa tu wakati wanatafuta kazi nchi za ng'ambo hasa Mashariki ya Kati.

Kwa upandE wake katibu mkuu wa vyAma vya wafanyakazi nchini Kenya Francis Atwoli Ametaka kubuniwa miji zaidi kwa lengo kupunzuza msongamano kwenye mji wa Nairobi na kubuni nafasi za ajira.