Mzee aliyeishi miaka 146 afariki dunia Indonesia

Mzee aliyeishi miaka 146 afariki dunia Indonesia

Raia wa Indonesia ambaye alidai kwamba alikuwa na umri wa miaka 146 – binadamu aliyeishi muda mrefu zaidi duniani – amefariki dunia kijijini mwake Java ya Kati.

Kwa mujibu wa stakabadhi alizokuwa nazo, Sodimedjo, aliyefahamika pia kama Mbah Ghoto (babu Ghoto), alizaliwa Desemba 1870.

Haya ni mahojiano yake na BBC alipokuwa na miaka 145 mwezi Septemba mwaka 2016.