Mshauri wa Trump kuachia ngazi

Gorka ataondoka siku chache zijazo
Image caption Gorka ataondoka siku chache zijazo

Taarifa kutoka Washington zinasema kuwa mmoja wa washauri muhimu sana wa Rais Donald Trump Sebastian Gorka anatarajia kujiuzulu nafasi hiyo.

Gorka mjuzi wa masuala ya usalama wa taifa anashutumiwa kuvaa medali aliyozawadiwa na kikundi kimoja kutoka nchini Hungary ambacho kina uhusiano na mfumo wa Kinazi.

Kabla ya kufanya kazi na Trump, Gorka alikuwa mhariri wa tovuti iitwayo Breitbart.