Castro ashuhudia maadhimisho ya mwisho ya wafanyakazi Cuba

Raul Castro ametangaza kuondoka madarakani mwezi Februari mwakani
Image caption Raul Castro ametangaza kuondoka madarakani mwezi Februari mwakani

Mamilioni ya raia wa Cuba wameshiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika sehemu maarufu ya iitwayo Havana Square na nyinginezo ikiwa ni ya kwanza tokea kifo cha Rais wa zamani Fidel Castro na ya mwisho kabla ya Rais wa sasa Raul Castro kuondoka madarakani.

Image caption Familia ya Castro imekua madarakani tokea mwaka 1976

Maadhimisho hayo yaliambatana na kuimba nyimbo mbalimbali, kubeba bendera, pamoja na kuvaa nguo zenye rangi ya bendera ya nchi.

Raul Castro anatarajia kuachia ngazi mwezi Februari mwakani, huku ikitazamiwa kuwa mwisho wa kizazi hicho madarakani.

Haijawekwa wazi ni nani atakayechukua nafasi hiyo.